Baraza la Meya la Wahamiaji wa Pittsburgh na Jamii za Kimataifa  Nakala ya Kutafsiriwa Mnamo Mei 6, 2021, Muungano wa All for All, ukiwa umepangwa na Global Switchboard,  ulifanya Mkutano wa Mameya wa wahamiaji wa Pittsburgh na jamii za kimataifa. Baraza hili lilijumuisha wagombea wanne wa kidemokrasia wanaogombea kiti cha Meya cha Pittsburgh; Mwakilishi  Ed […]

SWAHILI: Mayoral Forum by Pittsburgh’s Immigrant & International Communities, May 6, 2021 | The Global Switchboard | Hub
menu
Close


SWAHILI: Mayoral Forum by Pittsburgh’s Immigrant & International Communities, May 6, 2021

Baraza la Meya la Wahamiaji wa Pittsburgh na Jamii za Kimataifa 

Nakala ya Kutafsiriwa

Mnamo Mei 6, 2021, Muungano wa All for All, ukiwa umepangwa na Global Switchboard,  ulifanya Mkutano wa Mameya wa wahamiaji wa Pittsburgh na jamii za kimataifa. Baraza hili lilijumuisha wagombea wanne wa kidemokrasia wanaogombea kiti cha Meya cha Pittsburgh; Mwakilishi  Ed Gainey, Bw. Tony Moreno, Mayor Bill Peduto, na Bw. Mike Thompson. Lengo la baraza hili lilikuwa kuinua na kuweka kati sauti za jamii za wahamiaji na wakimbizi katika mzunguko wa uchaguzi uliotelekeza na kutenga masuala ya kipekee yaliyo muhimu kwa jiji wanamoishi wahamiaji na watu wa mataifa mengine. Uwezo wa watu kuishi katika jiji letu hutegemea sana hujumuishaji na uwezeshaji wa wahamiaji na watu wa mataifa mengine katika jiji hili bila kujali asili ya nchi, dini, lugha, hali ya kiuchumi-jamii, kabila, jinsia au ujinsia.

Maswali ambayo yaliwasilishwa kwenye baraza hili yalikuwa yamepangwa na wanachama wa Muungano wa All for All ambao wana uhusiano wa kishirika na kibinafsi na wahamiaji walioshi na uzoefu wa kimataifa jijini Pittsburgh. Baraza hili lilikusudiwa kwa watu wote wa Pittsburgh lakini lilitolewa hasa kwa wahamiaji wote na watu wa kimataifa wanaoita Pittsburgh nyumbani tunapoelekea kwenye uchaguzi mnamo Mei 18 na Novemba 2, 2021.

Ili kulifanya baraza hili kufikika kilugha, tumechagua maswali sita ambayo yanaonyesha maoni ya wagombeaji kuhusu masuala yanayohusiana na wahamiaji na watu wa kimataifa. Vigezo vya kuchagua swali vilizingatia uzito wa jibu ambalo kila mgombeaji anaweza kufanywa kuwajibikia ikiwa atachaguliwa kuwa meya. Majibu haya yamenakiliwa kwa mkono na kutafsiriwa na Global Wordsmiths. Rekodi ya baraza kamili, katika Kiingereza, inapatikana kwenye kituo cha YouTube cha Global Switchboard.

Kanusho: Muungano wa All for All HAUITHINISHI  yoyote ya misimamo hii ya sera ya wagombeaji wala kuithinisha yeyote wa wagombeaji wa kiti cha Meya cha Pittsburgh. Majibu yalioonyeshwa hapa HAYAJACHUNGUZWA kujulikana iwapo ni ya kweli. Ili kudumisha kutopendela upande wowote, Muungano wa All for All unatafsiri majibu ya wagombeaji bila kutoa maoni. Tunatarajia kuwa majibu haya yaliyotafsiriwa yatatoa makala zaidi kwa wapiga kura kufanya uamuzi sahihi.

Swali la #3 Vikwazo vya lugha hutoa hatari wazi na ya dharura kwa watoaji huduma na pia wahamiaji na wakimbizi katika mji huu. Pale ambapo ukalimani na tafsiri haitolewi, wahamiaji wengi walio na ufasaha wa chini wa Kiingereza hunyimwa ufikiaji wa kila kitu kutoka kupata leseni ya uendeshaji gari hadi kupata chanjo ya COVID-19. Kwa kuzingatia kuwa usaidizi wa lugha huhitajika chini ya Mada VI ya Sheria ya Haki za Raia na EO 13166, na pia Kanuni ya Mizinga ya Jiji la Pittsburgh, ni vipi ambavyo Uongozi wako utafanya ili kuboresha ufikiaji wa lugha  Pittsburgh na Jijini?

Mwakilishi Gainey: hilo ni mojawapo ya masuala ambayo ninazungumzia kuhusu ninapozungumza kuhusu kufaya kazi na jamii. Tunafahamu kuwa kwa kufanya kazi na jamii tunaweza kutoa watafsiri, lakini ni lazima tuwe na mtu ambaye anatuongoza hapa, ninadhani kuwa mojawapo ya mambo uliyosema kuwa yalikuwa muhimu ni COVID 19, kutojua pahali pa kwenda kudungwa sindano, kutojua pale ambapo hata walihitaji kupimwa ili kuona ikiwa walikuwa na COVID-19. Hapa ndipo uongozi wa mji huhitaji kufanya kazi kwa karibu na jamii zote, kila jamii, kutambua wanachohitaji. Na ikiwa wanahitaji wafasiri wa kuwasaidia kuelewa wanapopaswa kwenda ili kufanyiwa uchunguzi, au pale ambapo ni lazima waende ili kudungwa sindano, lazima tufanye kazi nao. Yote yanahusu kujenga uhusiano wa heshima na jinsi tunavyofanya kazi pamoja na niko tayari kufanya kazi nao, niko tayari kufanya kazi nao ili kuhakikisha kuwa wana watafsiri wanaohitaji na pia kuunda ajenda tunayoweza kuifuata.

Mr. Thompson: Ndio, vizuizi vya lugha  ni suala kuu. Nina mkimbizi Myahudi, hiyo ndiyo historia yangu, kutoka Austria, babu yangu alitoroka Viena, Austria baada tu ya Kristallnacht. Hivyo, ninahitimu kurudi Austria ikiwa ningependa uraia mara mbili, lakini, sizungumzi Kijerumani, sawa, hivyo ikiwa nilikuwa Austria kimsingi ningekuwa bawabu kwa sababu ni hayo tu unaweza kufanya ikiwa huzungumzi Kijerumani na ningepata matatizo sana kutembea karibu, ikiwa ningeishi pale, sizungumzi lugha vyema. Na nina shahada ya chuo, lakini sizungumzi lugha hii, hii ni kweli kwa watu wengi wanaokuja Pittsburgh. Ikiwa huzungumzi lugha hii, ni tatizo, sawa. Hivyo hakika unachohitaji ni mpango kama yalivyo nao majiji mengine, huduma ya kupiga simu ingekuwa bora, ambapo unaweza kupiga na kuna mkalimani anayepatikana, sijui ikiwa unahitaji mkalimani wa kila wakati kwa baadhi ya lugha zisizotumiwa sana zaidi, lakini hakika tungeshirikiana na, kuna baadhi ya huduma ambapo unapiga na kuna mkalimani anayepatikana na mtu huyo anakusaidia katika mchakato wote. 

Bw. Moreno: Lazima tuweke kipaumbele, ninajua katika utekelezaji wa sheria na katika idara ya polisi, huwa tunapambana kuwa na wakalimani na mara kwa mara huchukua dakika kadhaa, ikiwa sio saa, kuwasiliana na mkalimani ukiwa mtaani na muda mwingi ambao huwa tatizo kuu kwa kuwa hatupaswi kuwa tunaweka watu rumande kwa njia hiyo. Pia wanapohamia ujirani huu, lazima tutumie mfano wa wakimbizi wa kirusi baada ya vita baridi walipokuja kwenye kilima cha Squirrel, tayari walikuwa na watu ambao walizungumza Kiingereza na Kirusi, waliweza kuwapeleka katika nyumba ambazo walikuwa wamepanga, walikuwa na mpango wake, sasa hivi hatuna mipango hiyo tayari, au angalau hatuitumii kwa njia sahihi kwa sababu tunaona watu hawa wakiteseka. Nilikuwa Northview Heights na kulikuwa na mtu mmoja ambaye alikuwa akifanya ukalimani kwa watu kadhaa waliokuwa wakija katika hafla niliyokuwa nayo. Hivyo kwa kutazama hiyo ikitendeka na kwa kufahamu kuwa Beechview hupambana kupata ukalimani, tungeweza pia kuwapa teknolojia, simu nyingi za mkononi za kisasa na vipakatalishi huwa na uwezo wa kuingiza sauti kwake unapozungumza na kuzungumza tena sauti wanayozungumza

Meya Peduto: Hii ni sehemu moja muhimu ya Kukaribisha Pittsburgh, tuliweza kuunda hifadhidata ya watoa huduma wote tofauti walio katika Jiji la Pittsburgh, hivyo COVID ilipoanza, tuliweza mara moja kuwa na mikutano na watoaji huduma hawa. Pili, na kuwa kupitia Kampeni Tulivu ya Utunzaji tuliyoiendeleza. Sehemu ya pili ya hiyo ni kuwa pia tuliweza kuunda mikutano ya kila wiki kwa, sio tu wahudumu, lakini na jamii za wakimbizi na wahamiaji ili tuweze kujibu maswali moja kwa moja na kimaalumu. Na tatu, tuliunda kituo kipya cha uhamishaji wa lugha ambacho kimebadilisha na kuunda hati zetu zote muhimu kwa lugha kadhaa  kwa kuajiri mhusika mwingine na sasa 311 inaweza kuchukua maagizo na mahitaji, kulingana na lugha yoyote duniani. 

Swali la #4:  Kama meya, ni vipi ambavyo utafanya kazi na watu waliochaguliwa na jimbo, bodi ya shule na viongozi wengine wa eneo ili kuhakikisha kumudika na ufikiaji wa utunzaji bora wa mtoto na fursa za kielimu ambazo zinatoa jibu kitamaduni na kilugha kwa mahitaji ya wahamiaji na watoto na familia za wakimbizi?

Bw. Thompson: Kweli, hakika lazima tufanye kazi na bodi ya shule na viongozi wa jimbo. Ninadhani kuwa jambo tunaloweza kufanya ni kuzungumza [kuhusu] asili anuwai ya Pittsburgh. Pia, ikiwa utazungumza na watu walioshi hapa milele, wengi wao walikuja hapa kama wahamiaji na walikuja hapa kutoka sehemu zingine. Na ni lazima tuzungumze zaidi [kuhusu]  tulikotoka miaka iliyopita na tuone kinachofanana kati yetu, badala ya tofautiz etu. Mara nyingi sana, watu ambao ni wakimbizi au wahamiaji hushughulikiwa kwa njia tofauti, kama kwamba wao sio binadamu, wakati wao hakika ni binadamu sawa na Marekani ni taifa la wahamiaji. Na ni lazima tukumbuke kuwa  huo ndio msingi wa sisi ni nani.

Bw. Moreno: Hatuwezi hata kupata utunzaji wa watoto kwa wanawake wa rangi Nyeusi jijini Pittsburgh sasa hivi ili waweze kuinuka [kujiinua?] wenyewe kutoka kwa umaskini ambao wanaishi nao, hivyo hilo linapaswa kuwa kipaumbele hakika. Lazima tuhakikishe kuwa tunapanga haya na sasa unapojumuisha wahamiaji walio na tatizo la kuwasiliana, lazima tulete maendeleo ya masomo ya watoto, tuwe na walimu wanaozungumza Kiingereza, kwa kuwa nilipokuwa ninakua, nilimuuliza baba yangu ni kwa nini hakunifundisha Kihispania na alisema kuwa haikuwa vyema katika 1968 kwa watoto kujifunza Kihispania. Na niligundua hii kwa kuwa marafiki wangu wengi walikuwa Wameksiko, pia hawakuwa wakizungumza Kihispania, isipokuwa iwapo walikuwa na mzazi aliyekuwa akizungumza Kihispania tu. Hivyo wangewatafsiria. Hivyo tulipaswa kwenda katika kaya hizi na kujua jinsi wanavyowasiliana. Kwa kuwa wakati mwingi mzazi asiyezungumza Kiingereza hatajifundisha Kiingereza na ni lazima uwafundishe watoto ili wawasiliane na wazazi wao na wazazi wao wawasiane nao. Ikiwa tutapea hiyo kipaumbele na itakuwa rahisi kuishi na kisha unaweza basi kupata huduma wanazohitaji mapema katika mchakato wao wa elimu. 

Mayor Peduto: Mojawapo ya njia kuu ambazo tunaweza kutumia ili kuweza kuhakikishia, hasa vijana wetu wa Pittsburgh, fursa kupitia elimu ni kupitia kushawishi na kuboresha Kiingereza kama mipango ya Pili ya Lugha katika Shule za Umma za Pittsburgh na kupitia ufadhili kupitia jimbo la Pennslyvania. Kiingereza kama mpango wa Lugha ya Pili huwasaidia wahamiaji kuweza kuwaruhusu watoto kuweza kufundishwa sio tu kwa lugha ya Kiingereza, lakini pia kwa lugha yao ya nyumbani. Mjomba wangu alikuwa mtu aliyekuja nchini humu kutoka Italia, akiwa hawezi kuzungumza Kiingereza – katika wakati wake lugha hiyo haikuwa ikifundishwa. 

Mwakilishi Gainey: Kwanza, tunahitaji kufanya kazi na maafisa wetu wa jimbo kila wakati ili kuhakikisha kuwa wakati tunapeana pesa kwa kipengee kinachohusiana na utunzaji wa mtoto kuwa zinaongezwa, kwa  kuwa tunajua jinsi ilivyo muhimu. Pili, lazima tufanye kazi a wilaya ya shule. Lazima tufanye kazi na wilaya ya shule ili kuhakikisha kuwa tuna kikundi anuwai cha walimu ili elimu iwe ulimwenguni kote. Kwa sababu tunaelewa kuwa jinsi tulivyo na walimu wengi kutoka maeneo tofauti, ndivyo tutakavyojifunza zaidi. Tatu, tuna milioni mbili katika bajeti ya jiji ya utunzaji wa watoto ambazo bado hazijatumika. Lazima tutumie pesa hizo kwa utunzaji wa watoto ili tuendelee kuonyesha jiji la Pittsburgh kuwa tunaelewa manufaa ya kuwa na utunzaji wa watoto. Hivyo hayo ndiyo maeneo manne ambayo tunaweza kuongoza kama jiji.

Swali la #5:  Kulingana na Kituo cha Utafiti cha Keystone, wahamiaji jijini Pittsburgh wanawasilisha sehemu kubwa ya wamiliki wa biashara ndogo kuliko idadi yao ya uwiano jijini. Kulingana na Uchumi mpya wa Marekani, wahamiaji wana uwezekano wa asilimia 36 wa kuanzisha biashara kuliko wakaazi thabiti waliozaliwa nchini Marekani. Kwa kuzingatia uwezo mkuu wa kiuchumi wa wajasirimali wahamiaji wa Pittsburgh, ni vipi ambavyo usimamizi wako utasaidia wajasirimali wahamiaji wanaotamani kufungua biashara jijini Pittsburgh?

Mayor Peduto: Tunaifanya rahisi iwezekanavyo ili kuweza kuamua aina yoyote ya mpango unaopatikana kwa biashara ndogo. Hivyo, tunapofanya kazi na kampuni tofauti zilizoanzishwa na wahamiaji katika miaka saba iliyopita, baadhi ya vizuizi hivyo hakika vilikuwa tu katika kuelewa kilichokuwa kikipatikana katika kiwango cha eneo, jimbo, au kiwango cha shirikisho. Mamlaka yetu ya Maendeleo ya Mjini sasa yameunda duka linalouza aina nyingi za vitu na huduma, ili kuweza kimsingi kuondoa vizuizi na kukaribisha wageni. Hii imeturuhusu kuweza kuona kampuni mpya zinazoanzishwa na wahamiaji jijini kote. Kwa kufanya kazi pamoja na wahudumu wanaofanya kazi katika jamii, wameweza kutuelekeza kwa wale walio na nia ya kuanzisha biashara zao.

Bw. Moreno: Hii ndio maana wahamiaji huja Marekani, kwa sababu hapa ndipo unaweza kuja na upate Ndoto ya Marekani na uanzishe biashara yako. Babu yangu alianzisha biashara ya Uendeshaji Malori. Alifanikiwa sana na akaisaidia jamii yake. Hivyo unapowatazama wahamiaji wanaokuja hapa, hao ni sisi. Hawa ni watu wetu. Hawa ni binadamu wanaokuja. Tunahitaji kuifanya rahisi kwao kuanzisha biashara hizi ili wasiogope kwa sababu hawawezi tu kuingia dukani na kupata kazi zao.  Wanajua wanachotaka kufanya. Usimamizi unaotatiza katika utoaji Leseni na Ofisi ya Vibali tayari ni mgumu kwa watu waliopo wa Pittsburgh. Fikiria ikiwa utatatizwa na lugha na unajaribu kuyatekeleza mambo hayo. Inasababisha kuchanganyikiwa. Hivyo ikiwa tunaweza kuanzia pale na kuhakikisha kuwa vitu hivyo vinapatikana kwao pale ambapo wanaweza kuelewa na wanaweza kuifanya rahisi zaidi kuanzisha biashara yao na watii kama mtu yeyote yule, watakuja wengi na watafanikiwa ikiwa tutawapa fursa hiyo. Hayo ndiyo yanayohusu hii. 

Bw. Thompson: Inapendeza sana. Mojawapo ya mambo niliyotambua kwa muda ni kuwa Marekani ni chungu moto na huwa inapata Wamarekani wageni  kila wakati. Kila mmoja nchini Marekani anapaswa kwenda kwenye sherehe, ambapo tuna uraia na tunapata raia wageni. Hivyo lazima uulize, “Ni nani alitengeneza Google?” Ukiwauliza watu ni nani aliyetengeneza Google, ni Wamarekani wawili na hutambulika kama Wamarekani, lakini hasa ni wahamiaji. Na hivyo ingekuwa jambo nzuri kuona kitu kama mpango wa ushauri. Kwa sababu, wengi wa raia wetu wa Marekani waliokuja kutoka nchi zingine, wana tajriba, wamekuwa wakiipitia. Wametoka kwingine, kutoka nje ya Marekani na wana ufanisi hapa na hakika wanapaswa kuweza kusaidia kushauri wengine katika mpango rasmi uliosaidiwa  na Jiji la Pittsburgh. Sawa, kwa sababu biashara ndogo ya mhamiaji inaweza kuwa tofauti kidogo na biashara ndogo ya Mmarekani. Huenda usizifahamu sheria zote. Mambo hufanyika tofauti kidogo nchini Marekani kuliko yanavyofanyika katika baadhi ya nchi zingine. Na ingekuwa vyema sana kuwa na mpango unaokaribisha zaidi na mpango rasmi zaidi ungekuwa jambo bora la kuanza.

Mwakilishi wa Gainey: Ndio, asante. Tunafahamu kuwa biashara ndogo inatatiza katika jiji hili, imekuwa tatizo kwa miongo. Tunahitaji kupanua uchumi wetu. Na jinsi unavyopanua uchumi wako ni kupitia kuwekeza katika biashara ndogo. Tunahitaji kufikia fursa  na mtaji, kwa sababu bila fursa na mtaji, biashara ndogo haziwezi kukua. Lazima tubadilishe PLI, lazima tuiboreshe. Pesa ni wakati na wakati ni pesa. Na tunahitaji mfumo unaosonga haraka sana kuliko jinsi PLI  inavyosonga sasa hivi. Tatu, tunahitaji kuvunja mchakato wetu wa ununuzi ili tuwe na mikataba zaidi mahali kwingine ili wanabiashara na wajasirimali wadogo waweze kunadi. Na mwisho, tunahitaji kutoa usaidizi wa kiufundi. Kuna istilahi nyingi katika mikataba hii na kuelewa kamili jinsi ya kunadi kwenye miradi hii ambayo watu hawaijui. Hivyo, tunahitaji kuhakikisha  tunatoa usaidizi wa kiufundi na kuhakikisha tena, kuwa hilo ni eneo ambapo tungekuwa na wafasiri, ili kutusaidia kuvunja michakato hii na kuwasaidia kuelewa. Hivyo ndivyo unavyoendesha biashara ndogo katika Jiji la Pittsburgh.

Swali la #6: Miaka kadhaa iliyopita Muungano wa Sera ya Kitaifa wa Manispaa na Kituo cha Demokrasia maarufu ulileta mapendekezo 21 ya mbinu ambazo majiji yanaweza kutumia kupambana na wizi wa ujira, kumaanisha kuwa mwajiri anayekosa kulipa kiwango cha chini cha ujira na/au malipo ya muda wa ziada, au kukosa kulipa mfanyakazi chochote kile kwa muda aliofanya kazi. Mapendekezo yalijumuisha kutoa misaada kwa mashirika yasiyo ya faida ili kuchunguza madai au kusimamisha au kubatili leseni ya biashara inayojishughulisha katika wizi wa ujira. Taasisi ya Sera ya Kiuchumi imekadiria kuwa gharama ya wizi wa mishahara huwagharimu wafanya kazi wa ujira mdogo zaidi ya dola bilioni 50 kila mwaka nchini Marekani. Wizi wa ujira ni wa kawaida sana kati ya wafanyakazi wasio na hati, hasa katika mikahawa na tasnia za ujenzi. Kama meya, utafanya nini ili kuhakikisha kuwa wafanyakazi katika jiji la Pittsburgh, ikijumuisha wafanyakazi wasio na hati, wanalipwa wanachodai kwa kazi yao? 

Bw. Moreno: Hili ndilo eneo nililozungumzia kulihusu hapo mwanzo. Kwanza, lazima tulipe kipaumbele suala la kuwapa watu hawa hati wanazohitaji ili waweze kuanza safari yao ya uraia na wanaweza kuanza kwenda kufanya kazi na wasiogope hii. Biashara hizi huku nje hutumia hiyo kama silaha na kuwaweka watu hawa na kutowalipa wanachopaswa kupata, ila kuwalipa pesa kidogo na wanateseka. Hawawezi kuishi na ni unyanyasaji. Sio sawa kuhakikisha kuwa tunatumia Leseni na Ofisi yetu ya Vibali kwa njia hii, kwenda kuchunguza maeneo hayo. Huu ni uhalifu. Mara wanapopatikana wanapaswa kupelekwa kwenye idara ya polisi au ofisi ya DA na ni lazima watozwe faini, lazima washtakiwe. Na ni lazima iwe kipaumbele. Kwa kuwa imetendeka. Tunaiona ikitendeka sasa hivi. Unaenda popote jijini na unaona wahamiaji wakifanya kazi na unajua kuwa hawalipwi inavyopaswa. Ninajua binafsi kuwa hiyo inatendeka.

Bw. Thompson: Vyema, majiji na majimbo mengine hufanya kazi njema zaidi kuhusu kuwajulisha watu, kuweka nambari 1-800 za kupiga na kuripoti wizi wa ujira na kuchunguza wizi wa ujira. Lazima uulize ni sheria zipi zinavunjwa. Ikiwa hulipi ujira, mara kwa mara hiyo itakuwa sheria ya jimbo, hivyo mashtaka huenda yakahitajika kutoka kwa jimbo. Lakini unaweza kuwa na vitengo vinavyochunguza wizi wa ujira ambavyo huingia na kuzungumza na jamii za wahamiaji na pia jamii zisizo za wahamiaji, hii hutendeka kwa Wamarekani wote kwa bahati mbaya, sana katika jamii zilizotengwa, kama vile jamii za wahamiaji. Lakini, unawezakuwa na utekelezaji kamili wa suala hili. Nafikiri kuwa tunapaswa kupanga na maafisa wa jimbo na kuhakikisha kuwa sheria zinazovunjwa zinashtakiwa na tunahitaji hamasisho zaidi kuhusu suala hili.

Mwakilishi wa Gainey: Kwanza ni kuwa tuna kitu inaitwa Tume ya Ukaguzi wa Fursa Sawa na hapa pangekuwa mahali pazuri sana pa hii. Ili yeyote anayefanya biashara na Jiji linalojishughulisha na wizi wa ujira kutoka wakati huo kuendelea atazuiwa kufanya kazi jijini. Hatutakubali hiyo. Pili, tutafanya kazi na mashirika yasiyo ya faida – na mashirika yasiyo ya faida ya wahamiaji – ili kuzungumza kuhusu tunavyolenga mashirika na biashara ambazo wanahisi kuwa zinaleta wizi wa ujira ili tuhusishwe kutoka mwanzo na kuelewa wao ni nani. Na tatu, tutairipoti kwa jimbo, DA, ninamaanisha mwanasheria mkuu, ili kuhakikisha kuwa mashirika au biashara hizo zinawajibika kwa wizi wa ujira wanaoutekeleza. Hivyo hayo ndiyo mambo matatu. Kwanza, tutafanya kazi na Tume ya Ukaguzi wa Fursa Sawa, kwa sababu hiyo ni mbinu kuu ya kupalilia mashirika au biashara hizo zinazotekeleza wizi wa ujira. Pili, tena, tutafanya kazi na mashirika yasiyo ya faida  ili kuweza kulenga mashirika yanayofanya hivyo na yale yanayofanya hivyo tutaripoti kwa Mwanasheria Mkuu wa jimbo. Hivyo ndivyo tunavyoishughulikia chini ya Usimamizi wa Gainey. 

Meya Peduto:  Tunajivunia kushiriki katika kikozi hicho cha kazi pamoja na diwani Corey O’Connor. Mnamo Aprili 15, Siku ya Ushuru, nilipitisha Amri Kuu ambayo humtafuta kila anayejishughulisha na wizi wa ujira. Ni hatia. Ni sehemu ya sheria ya uhalifu. Unapomlipa mtu kisiri, hizo ni dola za ushuru ambazo kamwe hazirejei kujenga shule au kutengeneza mtaa, hizo ni familia zisizopata utunzaji wa afya au mengine. Na huangusha tasnia nzima. Kile ambacho ni lazima tuhakikishe ni kuwa kamwe haturuhusu wafanyakazi kuwa sababu ya mikataba kuwa chini. Kuwa kuna mahitaji sawa ambayo kila mkandarasi anafahamu kuwa lazima atimize, iwe ni ujira au mafao, au kifurushi chote tu.  Na wale ambao hakubaliani na wanalipa kisiri watakamatwa. 

Swali la #7: Kulingana na agizo la “Sera ya Polisi Isiyo na Upendeleo”, lililoanza kutumika katika 2014 na bado linatumika leo, Ofisi ya Polisi ya Pittsburgh haishirikiani, kushiriki habari, au kupanga na Ofisi ya Marekani ya Uhamiaji na Utekelezaji wa Sheria, iitwayo ICE, isipokuwa iwapo kuna agizo la mahakama lililoamrishwa na shirikisho.  Ikiwa utachaguliwa, ni ipi itakayokuwa sera yako kuhusu ushirikiano na ICE. 

Bw. Thompson: Ndio, sidhani kuwa tunapaswa kushirikiana na ICE. Ninadhani kuwa sera ya sasa ni sera nzuri na sera inayofaa. Kimsingi, ninamvulia kofia Bill Peduto, hiyo ndiyo sera inayofaa na hatupaswi kushirikiana na ICE.

Mwakilishi wa Gainey:  Hatupaswi kabisa kujihusisha na ICE. Tunapaswa kuwa tunawalinda raia wetu wahamiaji, hivyo hatupaswi kuwa na uhusiano wowote na ICE. Kazi yetu sio kutaka kuona watu wakiumizwa na ICE na kutengana kwa familia. Hiyo sio kuhusu Marekani, hiyo haitoi maelezo kutuhusu. Kinachotoa maelezo kutuhusu ni kuunganisha familia zetu na kuzileta pamoja na kuhakikisha kuwa wana maisha salama na sio maisha ambapo wanalazimika kuishi katika uwoga. Ninafikiri kuishi katika uwoga, hii huleta kiwewe kingi sana. Hatutaki kuleta kiwewe kwenye [kwa] raia wetu wa Pittsburgh. Kile tutafanya ni kuwa tutahakikisha tuna mfumo ambapo tunasaidia. Na ICE haina mfumo wa kusaidia, wana mfumo wa adhabu. Na hicho sio [kile] tunachokitaka katika jiji letu. Na hivyo, hatutafanya kazi na ICE, tutakachofanya ni kuwa tutafanya kazi na idadi yetu ya wahamiaji na kupata jinsi tunawezesha maisha yao. 

Meya Peduto: Kweli, kwa heshima ninatofautiana na alichosema Bw. Gainey. Alikuwa na fursa hiyo na alichagua kujiunga  na  Donald Trump  na kuunga mkono uthibitishaji wa mtandaoni. Uthibitishaji wa mtandaoni ni mpango kuwa ikiwa mfanyakazi kwenye mradi wa ujenzi au mahali kwingine hataonyesha hati, anapaswa kupelekwa kwa ICE. Unapopigia hiyo kura, unaunga mkono kufanya kazi na ICE na sio hiyo tu, unaunga mkono sheria katika jimbo la Pennsylvania inayoiamuru. Usimamizi wangu ulizuia mwingiliano kati ya idara yetu ya polisi na ICE. Kuna tofauti kubwa sana katika rekodi yetu. Mmoja alienda kinyume cha Donald Trump na akakumbana na tishio la kutupwa jela na Rais. Mwingine alimuunga mkono na akapitisha sheria, ili wafanyakazi wasio na hati warudishwe kwao.

Bw. Moreno: Ni suala la utekelezaji sheria. Hivyo, ikiwa tutahakikisha kuwa tunatekeleza sheria na ikiwa mtu atafanya uhalifu na ni mhamiaji asiye na hati, ICE hata haijalishi kwa sababu tunapaswa kuwa tunalinda jamii hizi. Unapoenda katika jamii, wana haki ya kulindwa kama mtu mwingine yeyote. Ikiwa mtu huyu aliyetekeleza uhalifu sasa amekuja chini ya sera ya uhamiaji, ukiukaji, basi tunapaswa kumfanyia nini? Tunahitaji kuhakikisha kuwa inarudi kwenye sera ya uhamiaji ya serikali ya shirikisho na kuwa inatumika pale. Sasa kwa kweli sisemi kuwa tunapaswa kuwa na ICE ikitawala katika maeneo yetu ya uhamiaji, samahani, maeneo yetu yanayowapa makazi wahamiaji, kwa kuwa hiyo itawaweka tu katika uwoga. Nilitazama hiyo ikitendeka katika nyanja ambazo babu yangu alikuwa anaongoza. Tunachopaswa kufanya ni kuhakikisha wako salama na kuwa ikiwa mtu anakiuka sheria na kufanya jambo asilopaswa kulifanya, kuwa inatumika ipasavyo. Sheria ya uhamiaji ni sheria. 

Swali la #11: Wahamiaji wanaokabiliwa na kufukuzwa nchini hawapewi wakili anayefadhiliwa na serikali kwa kuwa huenda wakawa katika mahakama ya uhalifu. Kama matokeo yake, wahamiaji ambao hawawezi kugharamia wakili huwa katika hatari ya juu sana ya kufukuzwa nchini kuliko wale wanaoweza. Kwa mujibu wa ukweli huu mkali, manisipaa 39 katika taifa nzima, ikijumuisha Philadelphia, yameunda mipango ya utetezi wa uhamishwaji inayofadhiliwa na umma. 

Je, unaamini kuwa kila mtu anayekabiliwa na kufukuzwa nchini ana haki ya uwakilishwaji wa kisheria? Ikiwa ndio, utajitolea kutoa fedha za jiji kulipia mpango ili kuhakikisha hii jijini Pittsburgh?

Bw. Moreno: Kabisa. Hii ni Marekani, unastahili kuwakilishwa. Hatuna wakili wa wahamiaji hapa jijini Pittsburgh, hakuna yeyote [wowote]  aliye mtaalamu, kuna wachache sana, samahani, watu wachache sana ambao ni wataalamu katika sheria ya uhamiaji. Hakuna hakimu wowote ambao ni wataalamu katika uhamiaji. Hivyo wanakutana na jambo ambalo liko juu ya uwezo wao. Ikiwa tutaanza tu kuvuta watu nje na kuwafukuza nchini, si vyema kwa sababu wakati mwingi huja hapa na wanaambiwa ni sawa. Hivyo ikiwa tunaweza kuwapa uwakilishaji, ikiwa wametekeleza uhalifu mbaya sana, tunapaswa kuweza kuwaweka katika mchakato wa kuwa raia wa Marekani kwa uwakilishaji. Tayari wanaishi hapa, wanafanya kazi, wanasitawi, familia zao ziko hapa. Hatupaswi kuwashughulikia kwa njia tofauti kuliko tufanyavyo tayari kwa mtu anayeishi nyumba iliyo karibu. Wanahitaji uwakilishwaji. Tunapaswa kuwaleta wataalamu hapa, kama Joe Murphy anayegombea kiti cha hakimu, hufanya hivyo sasa hivi jijini Clairton huwatafutia wanachohitaji na kuwawasilisha na hivyo ndivyo tunavyopaswa kufanya hivi. Hivi ndivyo tunavyoonyesha upendo kwa wahamiaji wetu.

Meya Peduto: Kabisa. Wajua, tulipoteza kizazi na tukarudi wakati wa uongozi wa Trump. Kizazi kilichopigania haki za wahamiaji, walio na hati na wasio na hati. Na kwa kufanya kazi na Casa San Jose  kwa mwaka uliopita kwa kesi za kibinafsi, kama unavyofahamu, mara nyingi tuliweza kupata mawakili ambao wangefanya kazi kwa malipo kidogo au bila malipo. Lakini iwe ni kuondoa haki au mipango ya wahamiaji au watoto wa wahamiaji, iwe ilikuwa kuongeza ada, iwe ilikuwa aina zingine zote za hatua iliyochukuliwa na uongozi wa Trump, tulipigana nazo kila wakati. Tuliwapeleka mahakamani na tulijiunga na mikutano ya kirafiki ili kuweza kulinda haki. Hizi ni haki ambazo watu walipigania kwa vizazi na ninatazamia kufanya kazi na uongozi wa Biden kuzirejesha na kuzipanua jijini Pittsburgh. 

Bw. Thompson: Hili ni jambo muhimu sana tunalopaswa kulifanya. Mara na tena. Watu huanguka kupitia nyufa. Wajua, mfumo wa kisheria sio wa walio na mali tu. Watu ambao ni masikini, wahamiaji, wakimbizi, wote pia wanastahili uwakilishaji wa kisheria. Ukitazama majiji mengine, kama Jiji la New York, wao hasa huajiri, kama, mawakili wa wapangaji ili kuwasaidia watu wanaokabiliwa na kutokuwa na makao, kufukuzwa nchini, kila aina ya masuala. Na mipango yetu kieneo haifadhiliwi vya kutosha, au haifadhiliwi kuhusu mpango huu. Wajua, una haki ya wakili katika kusikizwa kwa kesi ya uhalifu, haki, lakini sio lazima kwa masuala mengine ya kisheria na ni shimo kubwa katika jamii ya Marekani na ambalo tunahitaji kufanya kazi ili kuliziba. Ninamaanisha, kwa kweli ingekuwa katika kiwango cha shirikisho kurudi chini, lakini tunaweza kufanya mengi zaidi katika eneo.

Mwakilishi Gainey: Ndio, kabisa. Ndio maana, katika Jimbo nilipopigia kura kulinda miji ya patakatifu. Nilidhani kuwa hiyo ni muhimu kabisa. Na kisha ninapenda mfano wa wanachofanya Philadelphia na ninaamini kuwa tunaweza kufanya hivyo hapa Pittsburgh. Tunaweza kufanya kazi na mashirika yasiyo ya faida ya wahamiaji kuhakikisha kuwa kile wanachokifanya Philly, kwa kuwa tunaona kikifanya kazi, tunaiona ikisonga mbele, tunaiona ikifanya mambo makuu. Hivyo mwishowe, tunahitaji kuchukua mfano wetu na tunahitaji kuuleta Pittsburgh. Na tunahitaji kuutekeleza jijini Pittsburgh ili tuhakikishe kuwa tunatenda wala sio kutoa maoni tu. Na kando na kufanya kazi na mashirika yasiyo ya faida, mashirika yasiyo ya faida ya wahamiaji, ili kuhakikisha kuwa tuna mpango hapa, kuwa tunapata pesa zake, ninadhani Philly ina kama [dola] 100,000 ikiwa sio makosa. Lakini tungefanya hivyo hapa tu jijini Pittsburgh. Hiyo itawaruhusu watu kujua kuwa tunajitokeza kuilinda idadi yetu ya wahamiaji.